Lindi.Serikali imetoa kiasi cha Sh.50milioni kwaajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati ya Mkupama, kutokana na wananchi wa eneo hilo kutembea umbali mrefu zaidi ya km 15 kutafuta huduma ya afya katika kituo cha afya cha Ng'apa.
Baada ya kupata changamoto hiyo kwa muda mrefu wananchi hao waliamua kuanza ujenzi wa zahanati katika eneo la Mkupama, na serikali ikawaunga mkono kwa kuchangia Sh.50milioni ili kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la Zahanati hiyo ya Mkupama iliyopo Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi , mkazi wa Mkupama Bahati Muhidini amesema kuwa walikuwa wanatembea umbali wa km 15 kufuata huduma ya afya katika Kituo cha afya cha Nga'pa .
Mwihidini ameishukuru Serikali kwa kuweza kuwaunga mkono katika umaliziaji wa Zahanati hiyo ,licha ya hayo wanaiomba Serikali kuongeza watumishi wa afya katika zahanati hiyo.
"Zahanati hii imekuja kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu, lakini Zahanati hii inamuhudumu mmoja ambaye hawezi kutuhudumia wagonjwa wengi kwa wakati mmoja ,tunaiomba Serikali kuongeza wahudumu wengine ."Amesema Muhidini
"Sisi wananchi wa Mkupama tunaishukuru Serikali kwa kuweza kuunga mkono ujenzi wa Zahanati hii,tulikuwa tunateseka sana,unaumwa usiku huduma ya haraka hakuna hadi kituo cha afya cha Ng'apa, ambapo tulikuwa tunatembea umbali mrefu napia Serikali itusaidie kuongeza watumishi kwani huyu mmoja hawezi kuhudumia wagonjwa wengi kwa pamoja.Amesema Moza Haji.
Magret Poma muhudumu wa afya katika Zahanati hiyo ameiomba Serikali kumuongezea watumishi wengine pamoja na nyumba ya kuishi kwani anatoka mbali na ilipo Zahanati hiyo.
"Mim nahudumia wagonjwa wa nje tu ,na kwasiku nahudumia wagonjwa zaidi ya kumi ,naiomba Serikali iweze kunisaidia kuniongezea wahudumu wengine,kwani wagonjwa wanapokuwa wengi nashindwa kuwahudumia kwa wakati,napia naomba Serikali iweze kunitafutia nyumba ya kuishi naishi mbali, ikitokea mgonjwa wa dharula usiku inakuwa ngumu kufika kwa wakati ."Amesema Poma.
Mkuu wa Idara ya afya,Ustawi wa jamii na lishe Dk. Stanford Mwakatage amesema kuwa Zahanati ya Mkupama imeanza kujengwa kwa nguvu za wananchi,ambapo wananchi walichangia kiasi cha Sh.4milio
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.