Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary ametoa wito kwa wadau wa Maendeleo na wataalam wa Kilimo Lindi, kuhakikisha miradi yote ya maendeleo ya wahisani inakuwa endelevu kulingana na mpango na kuleta tija kwa jamii.
Ametoa wito huo Ofisini kwake Juni 6, 2025 alipokuwa anazungumza wakati wa kutambulisha shirika lisilo la kiserikali (SCAAP) linalofanya kazi na wakulima wadogo hususani wa mboga mboga ili kuondoa umasikini hasa maeneo ya kusini .
Bi. Zuwena Omary, akizungumza na wadau hao amesema, kumekuwa na miradi kadhaa ambayo inaanza vizuri lakini kabla haijafika mwisho inateteleka na tija iliyokusudiwa haionekani tena.
"Mtaalam ambaye eneo hilo ndiyo Mahusi hasa shirikiana na wadau kuhakikisha mradi unakwenda vizuri , hawa wahisani wanakuja kutokana na juhudi za serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan , hivyo tunakazi kubwa ya kusimamia miradi na kuleta tija kwa jamii"
Awali, akitambulisha mradi huo, Mkurugenzi wa Mradi Ndugu Adam K. Siwingwa amesema kuwa dhamira ya mradi huo kuwajengea uwezo wakulima wadogo kujihusisha na kunufaika na kilimo chenye tija , kuendeleza harakati zao za kuleta mabadiliko ya kisera na kusaidia vikundi taasisi zao kukua na ili kufikia haya shirika linazingatia uendelevu wa mazingira, usawa na uwajibikaji wa pamoja .
Kwa awamu ya kwanza, mradi huu unatarajiwa kutekelezwa katika Halmadhauri Nne ambazo ni Mtama, Lindi Manispaa , Ruangwa na kilwa ambapo wakulima vijana Elfu 20 wanaojishughulisha na bustani wanatarajiwa kufikuwa huku kila halmashauri ikiwa na vijana elfu 5. Aliongeza kusema Ndugu Adam Siwingwa.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Ndugu Mkungu Mwinjuma amesema, wamepokea maelekezo na wanakwenda kuyafanyia kazi ili mradi huo, uweze kuwa bora na kuleta tija wakati wote wa utekelezaji .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.