Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amepeleka kiasi cha shilingi bilioni 99 na milioni 300 kwa ajili miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Liwale.
Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa wilaya ya Liwale Godluck Mlinga amesema kuwa ndani ya kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, fedha zimesaidia kuchochea maendeleo ya wilaya hiyo kwa kasi .
Mhe. Mlinga amesema kuwa kwenye sekta ya afya walipata zaidi ya bilioni 3 na milioni 800 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya, Vituo vya afya Zahanati pamoja na vifaa tiba.
Amesema kuwa, serikali ya awamu ya sita ilitoa Bilioni 3 na milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari nne lengo likiwa kuinua na kuboresha elimu ya sekondari.
Aidha, Mhe. Mlinga, akitaja baadhi ya Mafanikio ambayo yamepatikana katika kipindi cha awamu ya 6 pamoja na ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mamlaka ya Ukusanyaji Mapato (TRA), Nyumba 2 za Afisa Tarafa katika tarafa ya Liwale Mjini na Kibutuka na ujenzi wa Chuo cha Ufundi stadi – VETA katika kata ya Makata ambapo jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 7.6 kimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Ameongeza kwa kueleza fursa mbalimbali zinazopatikana Wilaya ya Liwale pamoja na uwepo wa ardhi yenye rutuba ambayo inapokea kila aina ya kilimo hususani zao la korosho, ufuta, mbaazi, karanga na ufugaji.
Kihit Liwale yametokana na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025 na wao kama serikali kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya wamesimamia utendaji kuhakikisha yote yaliyopangwa yanafanikishwa kwa Mustakabali wa Maendeleo ya wana Liwale na Taifa kwa ujumla na pia,
Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutatua kero za wananchi na kuongoza viongozi wa ngazi zote wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wabunge na Madiwani kutatua changamoto za wananchi kwa kuwafikishia miradi ya maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.