Akizungumza na baadhi ya wananchi katika Hospitali ya wilaya ya Liwale mara baada ya kukagua huduma za kibingwa za macho zinazotolewa na timu ya madaktari kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi Sokoine, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt. Khery M. Kagya mekagua amesema kila baada ya miezi mitatu huduma hizi mbalimbali za kibingwa zitatolewa.
Huduma hiyo ilianza kutolewa siku ya jumatatu tarehe 11 Novemba ambapo hadi tarehe 15 Novemba 2024 wagonjwa wa macho zaidi ya thelathini na nne (34) wamefanyiwa operesheni ya macho.
Dkt. Kagya amesema Wizara ya Afya na wizara ya TAMISEMI zimeshirikiana kuweka taratibu za kutoa huduma za kibingwa kwenye ngazi ya hospitali ya wilaya kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi.
Aidha Dkt. Kagya ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Serikali yake anayoiongoza ya awamu ya sita kwa ujenzi wa miundombinu ya hospitali na vifaa vya kisasa, hii imesaidia sana kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma bora.
@samia_suluhu_hassan
@ikulu_mawasiliano
@ortamisemi;
@wizara_afyatz
H
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.