Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungo wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB ) ametembelea Shule ya wasichana Nachingwea kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo pamoja na kuona miundombinu ya Shule hiyo ikiwemo mfumo wa matumizi ya nishati safi ya kupikia .
Mhe. Waziri mkuu ameagiza kukamilisha kwa mifumo wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuachana na matumizi ya nishati chafu ya kuni ambayo siyo rafiki kwa afya na mazingira . Pamoja na agizo hilo ameagiza kuandikwa maombi ya kuboresha kwa baadhi ya miundombinu ya shule hiyo .
Akitoa majibu ya lini shule hiyo itaanza ktumia nishati safi ya kupikia mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mhandisi Chioanda Kawawa amesema taratibu za kumpata mzabuni zimekamilika ambapo makubaliano mwanzoni mwa mwezi wa Nne, 2025 mfumo huo utakuwa umekamilika kwakuwa mzabuni ameshapatikana .
Mara baada ya kuzungumza na wanafunzi Mhe. Waziri Mkuu ametoa Milioni 4 kwa wanafunzi ikiwema ni sehemu ya mchango wa chakula katika mfungo wa ramadhani na kwaresma .
Aidha, amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii kwani Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake wametimiza wajibu kwa kuboresha mazingira safi ya kusoma na kujifunzia hivyo jukumu la kila mwanafunzi kuhakikisha anasoma kwa bidii na kutimiza malengo .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.