Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Lindi katika kipindi cha Julai hadi Septemba imetoa taarifa ya ufuatiliaji na utekelezwaji wa miradi ya maendeleo kumi yenye thamani ya sh.Bilioni 20 katika sekta ya elimu,maji ,ujenzi na afya .
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi Bi. Asha Kwariko amesema wamefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi 10 ya Maendeleo na miradi miwili,wameikuta na dosari.
"Tumeendelea na ufatiliaji wa utekelezaji wa miradi 10 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 20 katika sekta za Elimu,Maji, Ujenzi na Afya."amesema Kwariko.
Amesema pia katika ufuatiliaji huo miradi 2 ilikutwa na mapungufu madogo madogo ambayo hatua mbalimbali zilichukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwashauri warekebishe mapungufu hayo.
Aidha, Bi. Kwariko ameeleza kuwa TAKUKURU Mkoa wa lindi imejipanga vyema kudhibiti vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaitarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba.
"Tunatarajia kuongeza juhudi ya kuzuia rushwa kwa kuhamasisha ushiriki wa wananchi kupitia nyenzo mbalimbali za uelimishaji umma katika kudhibiti vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ili wasirubuniwe kwa hongo au vishawishi vyovyote vile na kudhalilisha utu wao kwa kupokea rushwa ili wamchague kiongozi asiyefaa ama kujitoa katika kugombea au kupiga kura, na tayari tumeshafanya semina na makundi mbalimbali ikiwemo vijana, waandishi wa habari na viongozi wa dini tuna imani watafikisha ujumbe wa kupinga rushwa katika uchaguzi huu na tunaoutarajia mwakani" ameeleza.
Aidha, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi amewaomba wadau wote kuendelea kuwaunga mkono katia kuzuia vitendo vya rushwa kwa kutoa taarifa za viashiria vya rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.