Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unashiriki kikamilifu katika Maonesho ya Lindi Mining Expo 2025 yanayofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 14 Juni, katika Viwanja vya Madini, Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi.
Maonesho haya yanafanyika chini ya kauli mbiu:
“Madini na Uwekezaji, Fursa ya Kiuchumi Lindi – Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025.”
Kupitia banda maalum lililoandaliwa na TFS, wananchi na wadau mbalimbali wanapata elimu kuhusu shughuli kuu za wakala, zikiwemo:
• ✅ Uhifadhi wa misitu na rasilimali zake;
• ✅ Utalii wa ikolojia kupitia Hifadhi za Misitu za Taifa;
• ✅ Ufugaji wa nyuki na fursa za kiuchumi katika mazao ya nyuki;
• ✅ Taratibu za kisheria za biashara ya mazao ya misitu;
• ✅ Upandaji miti na umuhimu wa kuhifadhi mazingira;
• ✅ Matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia kwa lengo la kulinda misitu na kuboresha afya ya jamii.
Akizungumza katika maonesho hayo, mwakilishi wa TFS amesema ushiriki wa wakala huo ni sehemu ya jitihada za kujenga ushirikiano wa kimkakati kati ya sekta ya misitu na wadau wa madini, uwekezaji na mazingira kwa lengo la kuendeleza uchumi wa kijani nchini.
“Hii ni fursa muhimu kwa TFS kuelimisha umma kuhusu nafasi ya misitu katika ustawi wa taifa na kuchochea matumizi endelevu ya rasilimali kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo,” amesema mmoja wa maofisa wa TFS kwenye banda hilo.
Aidha, TFS inawahimiza wananchi wote wanaohudhuria maonesho hayo kutembelea banda lao ili kupata elimu, maarifa na fursa zinazopatikana kupitia sekta ya misitu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.