Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva amezindua mpango wa uwezeshaji vijana katika kilimo cha bustani katika mikoa mbalimbali ya Tanzania hususani Mikoa ya kusini chini ya shirika lisilo la kiserikali SCAAP.
Shirika lisilo la kiserikali SCAAP liliosajiliwa chini ya Sheria ya NGO ya Mwaka 2002 lenye usajili namba OONGO/R2/00367 lenye maskani yake Mbeya Uyole linalofanya kazi na wakulima wadogo wa bustani .
Akizindua mpango huo Mhe. Victoria Mwanziva ametoa wito kwa shirika la SCAAP katika kufanikisha mradi wa YEFFA swala la ushirikishaji wa viongozi na wananchi mara kwa mara ni muhimu sana kwani ndiyo msingi wa mafanikio ya miradi kama hiyo.
"Tunawataalamu mbalimbali katika ngazi za halmashauri, tushirikiane kufanikisha malengo na kuona matokeo ambayo yanaonekana waziwazi lakini siri kubwa ni ushirikishaji katika kila hatua ya utekelezaji ili matokeo yaonekane " DC Mwanziva .
Awali akiwasilisha lengo la mradi huo, Mkurugenzi wa SCAAP Ndugu Amani K. Siwingwa amesema mradi wa YEFFA unalenga kuongeza ajira kwa kuangalia fursa zilizopo kwenye minyororo ya thamani ya mazao mbalimbaliya bustani na kuhamasisha elimu ya kilimo biashara kwa vijana .
Ameongeza kuwa mradi huo utatekelezwa katika halmashauri ya Mtama, Lindi Manispaa, Ruangwa na Kilwa huku akitaja walengwa wa mradi ni wakulima vijana wanaojihusisha na shughuli za bustani katika mnyororo mzima wa mazao ikiwa na walengwa elfu 20 ambapo 80% ni vijana , kila wilaya inakuwa na angalau vijana elfu 5.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.