• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Utalii

VIVUTIO VYA KIHISTORIA KATIKA SEKTA YA UTALII

Katika mkoa wa Lindi vipo vivutio vya utalii vya asili na historia ya mkoa, taifa na dunia kwa ujumla, vivutio vinavyojitokeza bayana na kuwa kichocheo cha kukuza utalii vipo 19 kama ifuatavyo:-

  • Mlima wa Ilulu ulioko Nachingwea ambao ni mlima wa kihistoria unaothaminiwa katika mkoa wa Lindi hapa ndipo palikuwa makazi ya wamwera wakati wa safari yao ya kuingia mkoa wa Lindi baada ya kuvuka mto Ruvuma wakitokea Swaziland na baadae kutawanyika katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Lindi;
  • Fukwe za bahari zilizopo katika mwambao wa bahari ya hindi maeneo ya Kijiweni, Mchinga, Sudi, Kilwa;
  • Kaburi la Mchilima ambaye alikuwa mtawala wa jadi wa Mtama linalotumika kwa matambiko ambapo wananchi hukusanyika na kwenda kwenye kaburi lake na kumuomba aweze kuwaepushia mbali majanga, balaa n.k .
  • Godauni la watumwa Mchinga II ambalo lilikuwa linahifadhia watumwa waliotoka sehemu za bara na kuja pwani na kuhifadhiwa mahali hapo tayari kwa kusafirishwa kwenye maeneo ya visiwa vya Unguja, Madagascar na Re - union kwa ajili ya kufanya kazi kwenye mashamba ya matajiri.
  • Kaburi la Sister’s Walburg lililopo Nyangao. Huyu ni mjerumani wa kike aliyekuwa mwanzilishi wa hospitali ya misheni ya Nyangao ambayo kwa sasa hospitali hiyo imeingia ubia na halmashauri ya wilaya ya Lindi. Huyu aliuwawa na waingereza wakati akitaka kukimbia wakati wa vita kuu ya pili mwaka 1945 eneo la Ng’awa kuelekea Litingi umbali wa Km 4 kutoka mji wa Nyangao.
  • Mti wa Nyerere, katika kijiji cha Ntene kilichopo Kata ya Mnara, Tarafa ya Rondo, mti huu ni muhimu sana katika historia ya wakati wa uhai wa Mwalimu J. K Nyerere.  Umeitwa mti Nyerere kwa sababu hayati Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila alipofanya ziara ya kutembelea mkoa wa Lindi hususani katika halmashauri ya wilaya ya Lindi ilikuwa ni lazima afike katika mti huo.
  • Jiwe la mzungu, hili ni jiwe la asili kando kando ya bahari ya hindi katika kijiji cha Kijiweni, kata ya Mvuleni. Jina la Kijiweni limetokana na jiwe hilo ambalo lilikuwa pendekezo la mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji na Mreno Vasco da Gama ambaye alitawala nchi ya Msumbiji, Vasco da Gama alipigilia chuma katika jiwe hilo ikiwa ni ishara ya mpaka. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) alipinga jambo hilo na kusisitiza kuwa mpaka ni Mto Ruvuma ambao upo kusini mwa Tanzania, kutokana na msimamo huo ndio matokeo ya mpaka hadi leo hii kuwa ni mto Ruvuma.
  • Eneo alilopatikana mjusi mkubwa duniani ambalo  lipo katika kijiji cha Mnyangara, Kitongoji cha Namapwiya katika Tarafa ya Mipingo maarufu kwa Jina la Tendeguru. Kihistoria eneo hili ni muhimu sana kwani ni eneo ambalo mabaki ya mifupa ya mjusi mkubwa duniani (Dinosaur) au Dinosaria yalipatikana na kuchimbuliwa na hatimae kupelekwa Ujerumani kwenye jumba la makumbusho.
  • Msikiti na makaburi ya waarabu Sudi, umbali wa Km 12 kutoka kijiji cha Madangwa ambacho barabara kuu itokayo Mnazimmoja kuelekea Mtwara. Mji wa Sudi ni mji wa kihistoria kwa sababu ni mji wa siku nyingi na upo kando kando ya bahari ya hindi na ulikaliwa na waarabu ambao walikuwa wafanyabiashara ya watumwa ambako kwa sasa   yapo mabaki ya msikiti pamoja na makaburi ya waarabu.
  • Mikukuyumbu- (Kimambi) wilayani Liwale - Sehemu alikouawa Askofu Cassian Spiess mwaka 1905 na mtawala wa Wangindo aliyejulikana kwa jina la Abdallah Mchimae. Hivi sasa eneo hili linatumika kama sehemu ya hija kwa wakristo wa kanisa katoliki.
  • Mlima Nanungu – (Mlembwe) wilayani Liwale ambayo  ni sehemu ya matambiko na maombi ya kijadi.
  • Boma la zamani lililojengwa na Wajerumani mwaka 1905 (Makonjiganga- Liwale Mjini).
  • Pori la hifadhi ya taifa Selous  “Selous Game Reserve” ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani baada ya hifadhi ya Yellowstone iliyoko Marekani. Hifadhi hii ilianzishwa mwaka 1896 na Wajerumani ikiwa na ukubwa wa Km. za mraba 50,000. Jina la Selous linatokana na mwindaji namtaalamu wa mazingira akijulikana kwa jina la Captain Fredrick Courtney Selous aliyefariki katika mapigano ya vita kuu ya kwanza ya dunia mwaka 1917 katika eneo la Behobeho na kuzikwa ndani ya hifadhi. Ni hifadhi yenye wanyama mbalimbali na upo uwindaji wa kitalii ambao unaingiza fedha katika pato la taifa.
  • Mnara wa Nandete Kilwa ambako ni sehemu ilikoanzia vita ya Majimaji.
  • Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ikiwa ni kumbukumbu ya makazi ambayo ni mfano bora wa miji ya waswahili wa kale iliyojulikana kimataifa tangu karne ya 13 kabla ya kuzaliwa Kristu (BC). Kilwa Kisiwani ilianza kujitengenezea fedha/shilingi yake karne ya 11 mpaka karne 14. Wareno waliingia na kuimarisha ngome yao (Fort) na ndiyo iliyosababisha kuanguka kwa visiwa hivi viwili.  Hivi sasa Kisiwani na Songomnara ni kati ya hifadhi za kiutamaduni muhimu sana za Tanzania, hata zimeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya urithi wa Dunia ( World heritage)
  • Kilwa Kivinje ambao ni mji wa kihistoria na ndiyo iliyokuwa makao makuu ya eneo chini ya masultani wa Zanzibar na wakati wa ukoloni.
  • Mji wa Kilwa, ambao ulipata wageni kuanzia karne ya 9 mpaka karne ya 19, Ibin Battouta alitangaza Kilwa kuwa ni mji muhimu/mzuri duniani. Chanzo cha mji wa Kilwa ni miji ya Kisiwani na Songomnara ambayo ni miji muhimu iliyofikwa na wafanyabiashara (waswahili) wa Arabia, India na China kupitia bahari ya Hindi.
  1. Nyumba ya Samora Machel (Samora House) Nyumba hii ipo kilometa 34 kutoka makao makuu ya Wilaya ya Nachingwea (Farm 17). Nyumba hii ilitumika kama sehemu ya maficho ya aliyekuwa Rais wa Msumbuji hayati Samora Machel wakati wa kupigania  Uhuru wa Nchi yao.  Pia eneo hili lilitumika kama chuo cha  mafunzo ya wapigania uhuru katika nchi za kusini mwa Afrika ambazo ni Msumbiji, Angola, Afrika ya Kusini na Zimbambwe.
  • Wanyamapori na misitu ambayo ina vivutio vya wanyama na ndege wasiopatikana mahali pengine duniani.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.