MADAKTARI BINGWA NA BOBEZI 49 WA RAIS SAMIA AWAMU YA NNE YATUA LINDI.
Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma za afya za kibingwa na bobezi zilizoletwa na serikali katika hospitali zilizopo katika Halmshauri zao kwa lengo la kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora za kibingwa bila ya kutumia gharama kubwa za usafiri.
Katibu Tawala ametoa rai hiyo katika hafka fupi ya mapokezi ya madaktari bingwa na bobezi 49 waliowasili Mkoani Lindi kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi pamoja na kubadilishana uwezo na ujuzi wa kiutendaji na watumishi wengine wa afya waliopo katika vituo.
"Tunaendelea kuishukuru serikali kwa kusogezea huduma hizi kwa wananchi pamoja na dhamira yake ya dhati ya kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wake kwa kuboresha miundombinu ya utoaji wa huduma, kuajiri watoa huduma, kuhakikisha uwepo wa madawa na vifaa tiba katika vituo vya afya pamoja na kuleta timu za madaktari bingwa na bobezi ili wananchi waendelee kunufaika na kuboresha afya zao"
Aidha, RAS Zuwena amewataka watumishi waliopo kwenye vituo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa madaktari hao na wawe tayari kujifunza ili waweze kunufaika na kuboresha utoaji wa huduma na kuhamaisha wananchi juu ya uwepo wa huduma za kibingwa ili waweze kushiriki kikamilifu na kupata tija.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Bi. Juliana Chikoti ameeleza kuwa madaktari hao bingwa na bobezi 49 waliopokelewa wanakwenda kutoa huduma katika Hospitali za halmashauri 6 ambapo huduma watakazozitoa ni pamoja na magonjwa ya akina mama,
Huduma za Upasuaji,Ganzi na Usingizi,huduma za Uzazi na watoto wachanga,Kinywa na meno.
"Hii itasaidia huduma kusogea karibu zaidi na wananchi, kubadilishana uzoefu na kuongeza uwezo. Wananchi wakaribie kwa wingi katika kambi za madaktari bingwa ili waweze kupata huduma hizi"
Dkt. Nkunde Ramadhan, Daktari bingwa wa Upasuaji amesema"Ujio huu ni kwa ajiri ya watz ambao serikali imeona ni vyema iwaletee matibabu ya kibingwa na bingwa bobezi katika maeneo ambayo hawawezi kuyapata kirahisi na nina uhakika tunaenda kufikisha na kutoa huduma bora kwa masilahi ya watanzania wenzetu"MADAKTARI BINGWA NA BOBEZI 49 WA RAIS SAMIA AWAMU YA NNE YATUA LINDI.
Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma za afya za kibingwa na bobezi zilizoletwa na serikali katika hospitali zilizopo katika Halmshauri zao kwa lengo la kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora za kibingwa bila ya kutumia gharama kubwa za usafiri.
Katibu Tawala ametoa rai hiyo katika hafka fupi ya mapokezi ya madaktari bingwa na bobezi 49 waliowasili Mkoani Lindi kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi pamoja na kubadilishana uwezo na ujuzi wa kiutendaji na watumishi wengine wa afya waliopo katika vituo.
"Tunaendelea kuishukuru serikali kwa kusogezea huduma hizi kwa wananchi pamoja na dhamira yake ya dhati ya kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wake kwa kuboresha miundombinu ya utoaji wa huduma, kuajiri watoa huduma, kuhakikisha uwepo wa madawa na vifaa tiba katika vituo vya afya pamoja na kuleta timu za madaktari bingwa na bobezi ili wananchi waendelee kunufaika na kuboresha afya zao"
Aidha, RAS Zuwena amewataka watumishi waliopo kwenye vituo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa madaktari hao na wawe tayari kujifunza ili waweze kunufaika na kuboresha utoaji wa huduma na kuhamaisha wananchi juu ya uwepo wa huduma za kibingwa ili waweze kushiriki kikamilifu na kupata tija.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Bi. Juliana Chikoti ameeleza kuwa madaktari hao bingwa na bobezi 49 waliopokelewa wanakwenda kutoa huduma katika Hospitali za halmashauri 6 ambapo huduma watakazozitoa ni pamoja na magonjwa ya akina mama,
Huduma za Upasuaji,Ganzi na Usingizi,huduma za Uzazi na watoto wachanga,Kinywa na meno.
"Hii itasaidia huduma kusogea karibu zaidi na wananchi, kubadilishana uzoefu na kuongeza uwezo. Wananchi wakaribie kwa wingi katika kambi za madaktari bingwa ili waweze kupata huduma hizi"
Dkt. Nkunde Ramadhan, Daktari bingwa wa Upasuaji amesema"Ujio huu ni kwa ajiri ya watz ambao serikali imeona ni vyema iwaletee matibabu ya kibingwa na bingwa bobezi katika maeneo ambayo hawawezi kuyapata kirahisi na nina uhakika tunaenda kufikisha na kutoa huduma bora kwa masilahi ya watanzania wenzetu"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.