Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary na Timu ya menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, ikipokea taarifa ya ujio wa timu ya Madaktari bingwa na bingwa bobezi ambao wamewasili leo Septemba 15, 2025 mkoani Lindi.
Madaktari wanaongozwa na Eprahim Kafilimbi, Mratibu wa Madaktari bingwa na bingwa bobezi Mkoani Lindi.
Madaktari hao wanatarajiwa kutoa huduma za kibingwa na bingwa bobezi katika maeneo ya magonjwa ya wanawake na ukunga, watoto na watoto wachanga, upasuaji, usingizi na ganzi, magonjwa ya ndani pamoja na kinywa na maneo katika Hospitali za wilaya 6 zilizopo katika Mkoa wa Lindi huku Halmshauri ya Kilwa ikiwa na vituo viwili vya kutolea huduma hizo ambazo ni Hospitali ya Kinyonga na Kipatimu.
Aidha, Bi. Zuwena Omary, ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Mhe. Dakt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaleta madkatari hao kwa mara ya Nne Mkoa wa Lindi.
Wananchi wote mnakaribishwa .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.