Thursday 12th, December 2024
@MARENDEGU
Mwenge wa Uhuru ni chombo kilichoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo Taifa huru la Tanganyika.Mbio za Mwenge wa Uhuru zilianza rasmi Mwaka 1964 baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa nchi inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tangu kuanzishwa kwa Mbio hizi, Mwenge wa Uhuru umekuwa kichocheo kikubwa katika kuimarisha Uhuru wa Nchi, Umoja wa Kitaifa, Kudumisha Amani,kulinda Muungano na kuhamasisha maendeleo ndani na nje ya Taifa letu. Kuanzia mwaka 1964hadi mwaka 1992, Mbio za Mwenge wa uhuru zilikuwa zikiratibiwa na kusimamiwa Kitaifa na chama cha TANU na ASP baadaye CCM kupitia jumuiya yake ya umoja wa vijana.
Mwaka huu, 2021 utakuwa ni mwaka wa 29 tangu Mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe chini ya uratibu na usimamizi wa Serikali. Utaratibu huu ulitokana na abadiliko ya Kimfumo na Kidemokrasia baada ya nchi yetu kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, Mabadiliko hayo yalilenga kuthibitisha kuwa, Mwenge wa Uhuru hauna itikadi ya kisiasa,dini wala kabila bali ni mali ya Watanzania wote bila ya kujali tofauti zao
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.