Timu ya ufuatiliaji na Tathimini ya Mkoa wa Lindi imeendelea na ziara ya ufuatiliaji ukaguzi wa miradi ya maendeleo hasa miradi ya elimu ikiwa sehemu ya maandalizi ya kupokea wanafunzi kwa muhula mpya unaoanza Januari 13, 2026 kwa wanafunzi wa elimu msingi.
Timu hiyo inaongozwa na katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Mipango Ndugu Juhudi Mgalla akiambatana Mkuu wa kitengo cha Ufuatiliaji na tathimini, Mkuu wa kitengo cha Manunuzi, Mhandisi, na Daktari.
Timu hiyo imefanikiwa kutembelea miradi kadhaa na kubaini ubora na mapungufu mbalimbali ambayo yanapaswa kutatuliwa haraka kabla ya wanafunzi kuanza masomo Januari 13, 2025.




Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.