Sunday 11th, January 2026
@SEA VIEW BEACH RESORT - LINDI MUNICIPAL
“ Karibu katika mkoa wa Lindi, Asili ya Mjusi mkubwa na wa Kale kuliko mijusi yote mikubwa duniani na kituo sahihi kwa wawekezaji kufika na kutumia fursa zilizopo za Uwekezaji ”
Kazi kubwa tunayoitarajia hivi karibuni ni hatua ya kusambaza na kutangaza Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Lindi baada ya uzinduzi. Uzinduzi huu pamoja na mambo mengine unatarajiwa kutaambatana na:-
Baada ya kukamilika kwa mpango huu, kinachotarajiwa ni kuwawezesha wote wenye nia ya kuja kuwekeza katika mkoa wa Lindi, kujitokeza na kuonesha nia, kuchagua kipaumbele/vipaumbele kulingana na mahitaji yao na uzoefu wao na kuamua kuwekeza kulingana na Sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa.
Uongozi wa Mkoa wa Lindi unayo dhamira ya dhati ya kutekeleza mikakati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kukuza uchumi kupitia viwanda na kufikia uchumi wa kati nchini.
Kupitia ushauri wa kitaalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Kichumi na Kijamii (Economic and Social Research Foundation- ESRF) kuanzia mwezi Mei, 2019 mkoa wa Lindi umekuwa katika mchakato wa kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji (“Investment Guide”) ambao unatambua na kueleza kwa kina na ufasaha fursa zote za uwekezaji katika halmashauri zote sita za mkoa wa Lindi.
Kulingana na mpangilio uliotolewa na ESRF wakati wa kuanza zoezi hilo, mchakato wa kupata “INVESTMENT GUIDE” hauna budi kupitia hatua saba muhimu za kitaalamu kama ifuatavyo:-
Kwa sasa mchakato umefikia hatua ya sita ambapo ESRF waliandaa na kuwasilisha rasimu ya Mwongozo katika Sekretarieti ya Mkoa kutoa fursa kwa wadau kuupitia na kuhakiki taarifa zilizomo ili kujiridhisha na usahihi kabla mwongozo huo haujazinduliwa rasmi.
Mkoa kwa kushirikiana na ESRF uliandaa na kuwa na kongamano la siku moja tarehe 29 Agosti, 2019 lililoshirikisha wadau mbalimbali kwa ajili ya uhakiki wa mwisho wa usahihi wa taarifa zilizomo. Maoni ya wadau yaliyotolewa yamefanyiwa kazi na kuingizwa katika chapisho la mwisho. ESRF na uongozi wa Mkoa wameafikiana uzinduzi rasmi ufanyike siku ya tarehe 27 Novemba, 2019
Pamoja na mambo mengine chapisho la mwongozo linaweka bayana maeneo muhimu katika nyanja tatu zifuatazo:-
2. Vipaumbele vya uwekezaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni ambavyo ni:-
3. Sababu kumi na moja za kuwekeza katika mkoa wa Lindi zinabainishwa kuwa ni:-
Hali ya utangamano kisiasa na ulinzi wa uhakika na matukio machache ya uhalifu,
“ Hautajutia kuamua kuwekeza katika mkoa wa Lindi.”
Washiriki binafsi, taasisi/mashirika watakaopenda kushiriki katika kongamano la uzinduzi wa Mwongozo wanaombwa kuonesha nia kwa kujaza fomu ya ushiriki inayopatikana kupitia website ya mkoa wa Lindi www.lindi.go.tz na kutuma uthibitisho wa ushiriki kabla au ifikapo tarehe 25 November, 2019 kupitia barua pepe ps.ras@lindi.go.tz AU ras.lindi@tamisemi.go.tz nakala mipango@lindi.go.tz
Kupakua fomu ya ushiriki bofya hapa >>>> FOMU YA USHIRIKI (REGISTRATION Form).pdf
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.