Akitambulisha Mpango wa Afya Moja Dkt Sirilli Kullaya DCOP akiambatana na Mololo Noah kutoka @Ciheb na Richard Charles pamoja na Sarah kapanda kutoka PATH, mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na wadau mbalimbali wa maendeleo na Afya katika kusaidia uboreshaji, uimarishaji, uelimishaji na utatuzi wa changamoto mbalimbali zikiwemo za magonjwa ya mlipuko, amesema kuwa Afya Moja ni dhana ya kimataifa iliyoridhishwa na Mashirika kama WHO, FAO, OIFE na UNEP yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Sekta za Afya ya binafamu , Wanyama na mazingira ili kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza yanayoenea kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu (Zoonotic diseases ).
Kikao hicho cha siku mbili kimefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi Agosti, 2025 kikiwakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Afya, Kilimo, Wakala wa Maji RUWASA, Wataalamu wa Afya kutoka Hospitali ya Sokoine na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa sehemu ya Uchumi na uzalishaji pamoja na wadau kutoka PATH na Ciheb .
Dkt. Sirilli kullaya ameeleza kuwa sambamba na hilo afya Moja; itakabiliana na usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, usalama wa chakula, Changamoto za Afya zinazotokana na mabadiliko ya mazingira.
Aidha, Majukumu ya Afya Moja ,inajikita katika kuratibu shughuli za afya moja kuanzia ngazi ya taifa hadi vijiji, kuandaa mikakati na miongozo ya kukabiliana na milipuko ya magonjwa, kuunganisha wataalamu wa sekta mbalimbali - Madkatari, Wataalmu wa mifugo, Mazingira na kilimo .
Umuhimu wa afya moja unatokana na sababu ya utegemezi wa binadamu, wanyama na mazingira na hivyo tafiti zinaonesha 60% ya magonjwa ya binadamu yanatokana na maambukizi kutoka kwa wanyama, mabadiliko ya tabia ya nchi yanaweza kuchochea kuenea kwa magonjwa mapya na matumizi ya kemikali kwenye mazingira yanavyoathiri afya za binadamu na wanayama.
Mraibu wa mpango ngazi ya Mkoa Bi. Hadija Bakari ameshukuru hatua ya awali wa mpango huo kwani afya moja ni njia ambayo itahakikisha usalama wa afya kwa binadamu, wanyama na mazingira kwa ushirikiano wa kutatua changamoto kwa pamoja.
Naye mwenyekiti wa kamati Ndugu Ramadhani Hatibu akihitimisha kikao hicho, amewasihii wajumbe kuzingatia yote yaliyojadiliwa katika kikao hicho ili kuweza kuleta matokeo chanya katika utekelezaji wake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.