Uongozi wa Benki ya Ushirika Tanzania @cbtbank umeeleza dhamira ya kufungua Tawi la banki hiyo Mkoani Lindi ili kusaidia kutoa huduma kwa ufanisi kwa wanaushirika wake .
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ushirika Tanzania Ndugu Godfrey Ngurah alipokuwa anazungumza Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack alipotembelea kujitambulisha na kutoa taarifa rasmi.
Ndugu Godfrey ameeleza kuwa uwepo wa benki hiyo utaleta faida nyingi kwa wanaushirika hususani wakulima wa mazao ya biashara wa mikoa ya Lindi, Mtwqara na Ruvuma kwani itawawezesha wakulima kukopa kwa riba nafuu, kupata malipo yao kwa wakati , itawapunguzia usumbufu wa kulala kwa akunti zao, watapata faida kupitia hisa zao, kutoa fedha kupitia benki nyingine na kuweza kulipa wakulima kwa wakati mmoja kupitia mifumo bora ya mtandao .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ameipongeza banki hiyo kwa wazo lakufungua tawi Lidi na amewakaribisha kufanya uwqekezaji huo kwani uwepo wa benki hiyo kutaongeza chachu na faida nyingi kwa mkulima .
Kwa upande wa Mkoa wa Lindi tayari Chama kikuu cha ushirika Lindi Mwambao weshafungua akaunti kwa ajili ya kuanza kunufaika na benki hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.