Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva amekabidhi Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji (TACTIC) kwa mkandarasi HAMERKOP INTERNATIONAL LTD. JV KIKIM CONTRACTORS LTD, lro Julai 28, 2025 atakayetekeleza miradi mitatu katika manispaa lindi yenye thamani ya shilingi Bilioni 19.2.
Awali, Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Ndugu Juma Mnwele @mnwele alitaja miradi mitatu ya uboreshaji wa Miji ni ujenzi wa Kituo kikuu cha mabasi eneo la Mitwero, Soko Kuu kata ya Matopeni na barabara za lami km 5.3 ikiwemo barabara ya Mpilipili yote ikifadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia TACTIC.
Ameongeza kwa kusema mradi huo utatekelezwa kwa miezi 15 na hauna malipo ya fidia katika maeneo yote ambayo utatekelezwa .
Mara baada ya kukabidhi mradi huo kwa mkandarasi eneo la mradi wa Stendi Mitwero kata ya Rasibula Mgeni rasmi Mhe. Victoria Mwanziva amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi za miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Lindi zikiwemo hizo za miradi mitatu kwa pamoja.
Aidha , Mhe. Victoria ametoa wito kwa mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anasimamia vema kulingana na utalaamu na matakwa ya mradi .
" Serikali itakuwa karibu na kutupia jicho mradi huu ili kuhakikisha maono na azma ya Mhe. Rais inaonekana ikifanyika na hivyo kamwe hatutavumilia aina yoyote ya ubabaishaji utakao sababisha kazi hii kusuasua. Tutachukua hatua mara moja " Mhe. Victoria Mwanziva DC Lindi.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mwanziva amewataka TARURA (W) kusimamai mradi wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango kinachokubalika.
" Naelekeza pia TARURA kusimamaia mradi wa barabara kwa viwango vinavyotakiwa "
Wananchi wa Manispaa ya Lindi, wametumia fursa hiyo kuishukuru serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa fedha za miradi hiyo ambayo itakuwa chachu ya maendeleo .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.