Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amefanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa shule za Sekondari na Msingi Halmashauri ya Mtama .
Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt . Samia Suluhu Hassan ameipelekea Halmashauri hiyo Bilioni 7.8 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya Tano na miundombinu mingine kama vile madarasa na choo.
Katika ziara hiyo , Mhe. Telack amewataka mafundi na menejiment ya Halmashauri kuhakikisha wanasimamia vema miundombinu hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na thamani ya fedha iweze kuonekana.
Mhe. Telack amesema ,Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akileta fedha nyingi ndani ya mkoa wa Lindi ikiwemo Halmashauri ya Mtama, hivyo jukumu letu kuhakikisha miundombinu hiyo inatunzwa vizuri na watoto wanasoma vizuri .
@ortamisemi
@ikulu_mawasiliano
@zainabutelacky
@wizara_elimutanzania
@mohamed_mchengerwa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.