BILIONI 1.6 KUJENGA NA KUKARABATI MIUNDOMBINU YA NYUMBA .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi imepokea fedha zaidi ya Bilioni 1.6 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali chini ya ofisi hiyo.
Hayo yameelezwa na katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Ndugu Juhudi Mgallah akimwakilisha katibu
Tawala Mkoa wa Lindi katika ziara ya wakuu wa idara na vitengo ( Menejiment ) ya ukaguzi waujenzi na ukarabati
wa miundombinu hiyo .
Ndugu Mgallah, amesema miundombinu hiyo ni ujenzi wa fensi nyumba ya Mkuu wa Mkoa wenye thamani ya Milioni 520, ukarabati wa nyumba ya katibu Tawala wilaya ya Ruangwa na Liwale wenye thamani ya Milioni 213, ukarabati na ujenzi wa fensi nyumba ya wakuu wa sehemu (Idara) kwa thamani ya Milioni 758 na ununuzi wa mfumo wa viyoyozi kwa ajili ya ukumbi mkubwa wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wenye kwa thamani ya Milioni 118.
Aidha, viongozi hao wamekagua miradi hiyo na kutoa ushauri namna bora ya kutekeleza kwa kasi na viwango vinavyohitajika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.