BODI YA KOROSHO TANZANIA YAWAPIGA MSASA MAAFISA BIASHARA MKOA WA LINDI.
Mkurugenzi wa Masoko na Udhibiti Ubora kutoka Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Ndugu Revelian Ngaiza, leo ametoa mwongozo sahihi kuhusu masoko ya awali ya korosho sambamba na kuwakumbusha maafisa biashara kuhusu majukumu yao na umuhimu wa uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Leo Novemba 26, 2025, ikiwa ni siku ya pili ya mwendelezo wa kikao kazi cha Maafisa Biashara wa Mkoa wa Lindi, wataalam mbalimbali wameendelea kutoa elimu na kufanya uchambuzi wa kina kwa maafisa hao.
Wamehimiza kuzingatia misingi ya utumishi wa umma, uwazi, uadilifu na weledi katika kusimamia shughuli za maendeleo ya biashara na masoko.
Aidha, kikao hicho kimejadili changamoto zinazokabili sekta ya kilimo pamoja na mafanikio yaliyopatikana, huku kikielekeza nguvu zaidi katika mazao muhimu na fursa zinazochangia ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Lindi.




Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.