Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena amekabidhi na kuzindua Chanjo na vifaa vya utambuzi wa Mifugo Mkoa wa Lindi.
Akikabidhi na kuzindua Chanjo hizo Bi. Meena, amewataka wafugaji Mkoani Lindi kushiriki zoezi la chanjo ya mifugo ili kuimarisha ubora na thamani ya mazao ya mifugo katika soko na kuongeza uchumi wa wafugaji na nchi.
Bi. Meena, ametoa wito huo Julai 4, 2025 alipokuwa anazindua na kukabidhi rasmi chanjo na utambuzi wa mifugo kimkoa lililofanyika wilaya ya Kilwa na Lindi. Ambapo kwa wilaya ya kilwa jumla ya Mifugo Laki Tano Hamsini Nane Elfu na Mia Tisa Hamsini inatarajiwa kuchanjwa kati ya mifugo hiyo Ng'ombe 117,086 na kuku 2299,129 na Manispaa ya Lindi jumla ya mifugo Laki Moja Arobaini Tano elfu Mia Tano Kumi na Mbili.
Amesema changamoto kubwa inayosababisha wafugaji kupunguza thamani ya Soko la mazao ya Wanyama kimataifa ni pamoja na uwepo wa magonjwa yanayoathiri ubora wa nyama.
Bi. Meena, ameongeza kuwa, faida ya chanjo hizo ni pamoja na kusaidia kudhibiti magonjwa ya mlipuko kwa watu na wanyama, kuongeza uzalishaji wa mifugo, na kuongeza mapato ya Serikali kupitia Sekta hiyo.
Aidha, katibu Mkuu, ametoa wito kwa wafugaji kuendelea kuhamasishana kujitokeza kwa wingi ili kuchanja mifugo yao kwani kufanya hivyo kutachangia kwa kiasi kikubwa kutokomeza magonjwa ya mifugo katika mkoa na nchi kwa ujumla.
Kupitia zoezi hilo Serikali itachangia Shilingi 500 na mfugaji Shilingi 500 kwa ajili ya chanjo ya ng'ombe, Shilingi 300 kwa chanjo ya Kondoo na Mbuzi huku chanjo hiyo ikitolewa bure kwa wafugaji wa kuku.
Kwa upande wa wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva ambaye Mkuu wa Wilaya hiyo, amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hasssn Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chanjo hizo za ruzuku.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.