Katika kuunga Mkono mpango na juhudi za serikali za kuibua vipaji na kukuza sekta ya Michezo nchini, Benki ya CRDB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa Sare za Michezo kwa timu ya UMISSETA ya Mkoa wa Lindi kwaajili ya Maandalizi ya Mashindano ya UMISSETA Taifa yanayotarajiwa kuanza mapema mwezi Julai Mkoani Iringa.
Akipokea Jozi hizo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Katibu Tawala Msaidizi eneo la utawala na raslimali watu Mkoa Ndugu Nathalis Linuma ameishukuru Benki ya CRDB kwa msaada huo na kuahidi kuwa timu hiyo itafanya vizuri katika Mashindano hayo na kurudi na ushindi.
"Nitumie fursa hii kuishukuru Benki ya CRDB kwaniaba ya katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary kwa msaada wa jozi hizo ambazo imeipa timu hamasa ya kufanya vizuri na tuahidi, tunakwenda kufanya vizuri na kurudi na ushindi " Ndugu Nathalis Linuma.
Kwa upande wake kaimu Meneja wa CRDB Kanda ya Kusini Ndugu, Alpha J. Mhagama ambaye Meneja Mahusiano Kitengo cha Serikali CRDB kanda ya Kusini akiambatana na Meneja wa CRDB Lindi na maafisa wa Benki hiyo, amesema vifaa hivyo ambavyo vimekabidhiwa, nisehemu ya utaratibu wa Banki hiyo ya kusaidia matukio ama maswala mbalimbali ya kijamii ikiwemo michezo, lengo kuongeza chachu ya maandalizi ya timu hiyo ya UMISSETA Mkoa wa Lindi kufanya vizuri na kuchukua ushindi.
" Hatuendi kushiriki bali tunakwenda kushindana, kyshinda na kurudi na ushindi, nitarydi tena hapa kutoa zawadi kwa wale watakaorudi na ushindi " Amesema ndugu Mhagama.
Naye Afisa Elimu Mkoa wa Lindi Mwalimu Josephy Mabeyo amewasisitiza wanafunzi na walimu wa timu hiyo ya Mkoa kwenda kudumisha nidhamu wakati wote wa mashindano na nje ya mashindano .
"Nawasihii sana wanafunzi, mkawe na nidhamu wakati wote , nidhamu, nidhamu nidhamu muhimu sana katika kila jambo Waalimu wenu naamini watawasimamia vizuri sana " Mwalimu Kayombo -Elimu Mkoa.
Michezo ya UMISSETA kitaifa yanatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 7, 2025 Mkoani Iringa ambapo timu za Mikoa mbalimbali zitakutana kwa mashindano hayo.
Makabidhiano ya vifaa hivyo yamefanyija Juni 4, 2025 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Lindi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.