Wadau wa sekta ya madini katika mkoa wa Lindi wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa hatua madhubuti alizochukua katika kuboresha sekta ya madini, hatua ambazo zimewanufaisha wachimbaji wadogo na wanawake nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa Wachimbaji Madini Wanawake, Bi. Kuluthumu Runje, alisema sera mpya za madini zimevutia wanawake wengi kushiriki katika uchumi wa madini, tofauti na hali ilivyokuwa miaka ya nyuma.
“Ukienda migodini siku hizi utakuta wanawake wengi pamoja na vijana, jambo linaloonyesha jinsi mazingira ya uchimbaji yalivyoboreshwa—kuanzia upatikanaji wa vifaa hadi miundombinu bora,” alisema Bi. Runje.
Naye Katibu wa Umoja wa Vijana Wachimbaji Madini (UVIWAMA), alieleza kuwa jitihada za serikali kuipa sekta ya madini kipaumbele zimesaidia vijana wengi kujiajiri na kujipatia kipato kupitia uchimbaji mdogo.
Wananchi na wadau wengine wametakiwa kuendelea kuiunga mkono serikali katika juhudi hizi ili kuhakikisha sekta ya madini inaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi nchini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.