FORLAND YATAMBULISHA MRADI WA USIMAMIZI ENDELEVU WA MISITU NA ARDHI.
Timu ya FORLAND ikiongozwa na Ndugu. Michael Hawkes ambaye ni mshauri Mkuu wa mradi imetembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kukutana na Timu ya wataalamu Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na uzalishaji Ndugu.Mwinjuma Mkungu, kwa ajili ya kuutambulisha rasmi mradi wa usimamizi endelevu wa misitu na ardhi.
Utambulisho wa mradi huo umefanyika katika ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Julai 21, 2025.
Akiutambulisha mradi huo Ndugu. Michael Hawkes amesema ,mradi unalenga kuimarisha maisha ya wananchi kupitia matumizi bora ya ardhi na rasilimali za misitu kwa njia shirikishi.
Aidha, kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Ndugu. Mwinjuma Mkungu, mara baada ya mjadala wa kuutambulusha mradi ameipongeza timu ya FORLAND kwa dhamira yao ya kutekeleza mradi wenye lengo la kusisitiza matumizi bora ya ardhi na rasilimali za misitu ambayo itaimarisha maisha ya wananchi na hivyo viongozi wa Mkoa wa Lindi umeahidi kushirikiana kikamilifu ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huo .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.