• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

GULIO LA BIDHAA ZA USINDIKAJI NA USHONAJI KUCHAGIZA USTAWI WA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI MKOANI LINDI.

Posted on: November 2nd, 2024
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) ameliagiza Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kutengeneza mashine za kuchakata mwani na kukamua mafuta ya ufuta kwa wajasiliamali wa Mkoa wa Lindi walioko katika vikundi kwa kutumia Mfuko wa NEDF ili waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

Vilevile, ameliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) kuhakikisha Wajasiliamali hao wanapata nembo ya ubora na "bar code" ili bidhaa zao ziweze kushindana katika soko la kimataifa kama EAC na AfCFTA.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Novemba 02, 2024 alipokuwa akizindua Gulio la Bidhaa za Usindikaji, Ushonaji na Fursa za Biashara Mkoa wa Lindi linalofanyika kuanzia tarehe 01 hadi 03 Novemba 2024 Mkoani humo yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "ulipo ndipo walipoanzia".

Aidha, Waziri Jafo pia ameahidi kuwa Wizara yake itashirikiana na uongozi wa Mkoa huo katika kuweka mazingira bora ambayo yatawavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuanzisha viwanda kulingana na malighafi zinazopatikana katika mkoa huo ikiwa ni utekelezaji wa Programu ya Viwanda (2025- 2030) kwa lengo la kuongeza ajira na kukuza uchumi kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kuusaidia Mkoa huo kupata Viwanda vya kuchakata mazao mbalimbali ikiwemo mafuta ya Ufuta unaopatikana kwa wingi katika mkoa huo pamoja na viwanda vya kuchakata bidhaa za mwani .

Naye Mzee wa Kimila wa Mkoa wa Lindi Bw. Abdallah Hamis Livembe akimvisha vazi la Kimila la Utawala (Umwenye) kama ishara ya mtawala wa Mkoa huo amemuomba Waziri Jafo kuipa Lindi kipaumbele katika kuanzisha Viwanda ili kuongeza ajira na kukuza uchumi wa Mkoa huo na kufuta jina la "Mkoa wa nyuma kimaendeleo".

Akizindua Soko Mtandao (e-Soko) katika Gulio hilo Waziri Jafo ameuelekeza Mkuu wa mkoa huo wa Lindi kuendesha Gulio hilo kila mwezi kwa kushirikiana na Tantrade na kulitangaza ili lifahamike na kuvutia wajasiliamali kwa kushiriki kuuza na kunua bidhaa mbalimbali huku akiwataka Watanzania kupenda kununua na kutumia bidhaa zinazotengenezwa nchini.

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo(Mb) akivishwa vazi la kimila la umwinyi (Umwenye) wa Mkoa wa Lindi na Mzee wa Kimila Mzee Abdallah Hamis Livembe kama ishara au Mtawala wa Mkoa huo wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya kwanza ya gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi, Novemba 02,2024.
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo(Mb) akitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiliamali kuona bidhaa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya kwanza ya gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi, Novemba 02,2024.
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akizungumza wakati akizindua Maonesho ya kwanza ya gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi, Novemba 02,2024.
 
Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo(hayupo pichani), akizungumza wakati akizindua Maonesho ya kwanza ya gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi, Novemba 02,2024.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack,akizungumza wa uzinduzi wa Maonesho ya kwanza ya gulio la bidhaa za usindikaji na ushonaji Mkoani Lindi, Novemba 02,2024.


Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.