HALMASHAURI, TAASISI ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI ZATAKIWA KUIMARISHA HUDUMA KWA WAJASIRIAMALI MKOANI LINDI
Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva, Mkuu wa Wilaya ya Lindi amezitaka taasisi zote zinazohusika na sekta za viwanda, biashara na uwekezaji mkoani Lindi kuhakikisha zinatoa huduma bora kwa wafanyabiashara, ikiwemo kutoa elimu ya biashara na uwekezaji pamoja na kuwatembelea mara kwa mara katika maeneo yao ili kuongeza motisha na kuimarisha shughuli zao.
Aidha, amezitaka taasisi zinazohudumia wajasiriamali wadogo kama SIDO kuendelea kutoa elimu na mafunzo ya ujasiriamali pamoja na kuwawezesha kuzalisha bidhaa bora zenye ushindani katika soko, ili kukuza biashara zao na kuongeza vipato.
Vilevile, amezitaka Halmashauri kuhakikisha zinazingatia sheria na taratibu katika kusimamia upatikanaji wa mikopo ya 10% ili wajasiriamali wanaostahili waweze kunufaika na mikopo hiyo, hivyo kuchochea fursa na maendeleo ya sekta ya biashara katika mkoa wa Lindi.





Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.