• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

HAYATI MZEE MKAPA NI MFANO WA KUIGWA KWA MCHANGO WAKE KWA TAIFA: RAIS MWINYI

Posted on: July 23rd, 2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Hayati Mzee Mkapa atabaki kuwa mfano wa kuigwa kwa kizazi cha sasa na kijacho kutokana na mchango wake mkubwa katika kujenga misingi ya maendeleo, utawala bora na ustawi wa Taifa. Amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijenga nguzo muhimu za umoja wa kitaifa, Muungano, amani na mshikamano wa Watanzania, pamoja na nafasi ya Tanzania katika bara la Afrika na ulimwenguni.


Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Ibada Maalum ya Kumbukumbu ya Miaka Mitano ya Hayati Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanyika leo tarehe 23 Julai 2025 Lupaso, Wilaya ya Masasi, Mkoa wa Mtwara.


Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amekumbusha kuwa Hayati Mzee Mkapa alikuwa muumini wa ujamaa na uchumi wa soko unaoongozwa na sekta binafsi, lakini pia alihakikisha kuwa maendeleo yanawanufaisha wananchi wote bila ubaguzi. Ameeleza kuwa Hayati Mzee Mkapa ndiye aliyeanzisha Dira ya Maendeleo 2025, ambayo imekuwa chombo muhimu katika mageuzi ya maendeleo, na mafanikio yake yamekuwa msingi wa kuzinduliwa kwa Dira mpya ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.


Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito kwa viongozi wa dini, wanasiasa na wanahabari kuwa sehemu ya kulinda na kuendeleza tunu ya amani kama njia ya kumuenzi Hayati Mkapa. Amesema kuwa Watanzania wanayo sababu ya kujivunia viongozi waliopo ambao wanaendeleza maono ya viongozi waasisi na kuipeleka Tanzania mbele katika nyanja zote za maendeleo.


Rais Dkt. Mwinyi alizuru kaburi la Hayati Benjamin William Mkapa na kuweka shada la maua, akiongozana na Rais Mstaafu wa Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi, na Mkewe pamoja na Mjane wa Hayati Mkapa, Mama Anna Mkapa. Hayati Mzee Mkapa alifariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 24 Julai 2020 akiwa na umri wa miaka 81, jijini Dar es Salaam.


Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TAHADHARI YA MATAPELI WA MTANDANI

    September 03, 2025
  • MKOA WA LINDI WAJIPANGA KUFIKIA DIJITI MOJA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI NA WATOTO WACHANGA

    August 30, 2025
  • WANANCHI ZAIDI YA 2800 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MTAMA- LINDI

    August 29, 2025
  • AFYA MOJA NA MPANGO WA UDHIBITI NA USAMBAZAJI MAGONJWA YA MLIPUKO

    August 28, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.