Mwenge wa Uhuru 2025 umeridhia kuweka jiwe la Msingi kituo cha Afya Pangaboi kilichopo kata ya Nachunyu.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho Comred Ismail Ali Ussi ameridhia kuweka jiwe la msingi mradi huo ambao umezingatia vigezo na thamani ya fedha .
Komred Ismail Alli Ussi ametumia fursa hiyo kuwasihii wananchi kulinda miundombinu ya kituo hicho ambacho kinatoa huduma muhimu zikiwemo upasuaji huku akiwataka kuzingatia kanuni za Afya na kuepuka vitendo vya rushwa.
Amewataka kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi Mkuu wa 2025 ili kuchagua viongozi bora . Mradi huu umegharimu kiasi cha Tsh Milioni 500 fedha kutoka Serikali kuu.
Kituo cha Afya Pangaboi kinatajwa kuongeza kasi ya utoaji wa huduma ya afya kwa wakazi wa Nachunyu na viunga vyake kwani kimeondoa kero ya wananchi kutembea umbali mrefu kupata huduma hiyo kwa wakati .
Awali, Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya Mtama kwa mradi huo muhimu .
Mkoa wa Lindi, Mwenge wa uhuru 2025 umeanza mbio zake katika Halmashauri ya Mtama Mei 26, 2025 . Mei 27, 2025 unatarajiwa kuwasili Lindj Manispaa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.