Kamati ya Siasa Mkoa wa Lindi ikiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Daudi Msungu akiambatana na kamisaa Mhe. Victoria Mwanziva imetembelea na kukagua miradi kadhaa inayotekelezwa ndani ya Manispaa ya Lindi ikiwa ni utaratibu wa kawaida kila baada ya robo mwaka , kuona namna Ilani ya CCM inavyotekelezwa Nchini kote.
Baadhi ya miradi ambayo imetembelewa na kukaguliwa pamoja katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ni upanuzi wa usambazaji wa huduma ya maji kilangala wenye thamani ya zaidi ya Milioni 500, ujenzi wa Zahanati, Ujenzi wa Shule ya ghorofa yenye thamani ya Bilioni 1, ujenzi wa Shule ya Sekondari yenye Thamani ya Milioni 560 .
Katika ziara hiyo wajumbe walipata taarifa kutoka kwa mamalaka hudika zinazosimamia miradi na kila mbacho wananchi wanakizungumza kuhusu miradi hiyo. wananchi wameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miradi hiyo inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Aidha kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa namna ambavyo imeipelekea fedha nyingi Manispaa ya Lindi kwa ajili ya Shughuli mbalimbali za maendeleo.
Akihitimisha ziara hiyo MNEC Msungu amempongeza Mkuu wa wilaya hiyo na viongozi wote wa Halmashauri wakiwemo waheshimiwa madiwani na Mkurugenzi Mtendaji kwa usimamizi uliotukuka katika kufanikisha miradi hiyo mikubwa .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.