Kamati ya msaada wa kisheria imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli hiyo iliyodumu kwa muda wa siku 10 ndani ya mkoa wa Lindi tangu ilipozinduliwa Februari 19, 2025 wilyani Ruangwa na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Kampeni hiyo imefanya kazi katika halmashauri zote za Mkoa wa Lindi ikiwa imezifikia kata 74, vijiji 163, Mitaa 59 na kufanya jumla ya mitaa na vijiji 222.
Kampeni ilijikita katika kutoa huduma ya elimu ya Masuala ya kisheria , haki za binadamu na utawala bora, haki za watu wenye mahitaji maalum , ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto, ndoa , Miradhi na wosia, Ardhi, ajira na mahusiano kazini.
Mratibu wa kampeni hiyo Mkoa wa Lindi Ndugu Daudi Murumbe amasema zoezi la kutoa msaada wa kisheria Mkoani Lindi limefanyika kwa mafanikio kwani jumla ya wananchi laki 121,483 walifikiwa na huduma, huku wanaume wakiwa Elfu 55,462 na wanawake elfu 66,021 .
Ndugu Daudi ameeleza ipo migogoro ambayo iliweza kutatuliwa papo kwa papo na mingine iliendelea kushughulikiwa. Ametoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi , Katibu Tawala Mkoa na kamati ya maandalizi kwa ushirikiano ambao umesaidia kukamilisha zoezi hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amepongeza utaratibu huo ambao umeleta mafanikio katika mkoa wa lindi , amewasihii kuweka misingi imara ambayo itasaidia wanancbi kuendelea kupata huduma hiyo kwa urahisi.
@katibanasheria_
@mslegalaidcampaign
@humanrightstz
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.