Wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Kibutuka, Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, wameibuka washindi wa nafasi ya kwanza katika kipengele cha Biological Science kwenye Mashindano ya Young Scientist Tanzania yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Washindi hao, Musa Said Mwomboka (Kidato cha Nne) na Rashidi Abdala Njumbuke (Kidato cha Tatu), waliunda timu iliyoiwakilisha Kibutuka Sekondari na kuibuka kidedea kati ya washiriki 90 waliowasilisha miradi 45 kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini.
Akizungumza baada ya kutangazwa washindi, mwalimu wao, Juma Likana, alisema ushindi huo si tu heshima kwa Kibutuka Sekondari bali pia ni hamasa kwa wanafunzi wengine kuamini uwezo wao katika ubunifu na sayansi licha ya changamoto za mazingira.
Ushindi huo unatarajiwa kuleta manufaa kadhaa ikiwemo kuitangaza shule kimkoa, kitaifa na kimataifa, kuonesha
jitihada za walimu na wanafunzi katika taaluma na uvumbuzi, pamoja na kuisaidia jamii kutunza afya ya ngozi kwa kutumia bidhaa asilia badala ya vipodozi vya viwandani.
Aidha, ushindi huo umewajengea wanafunzi hao ujasiri na kujiamini kuwa wanaweza kufanya mambo makubwa, na hivyo kuongeza hamasa ya kujifunza zaidi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.