KILWA YANG’ARA NA MIRADI YA ZAIDI YA BIL 45.
Timu ya Watalaam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi ikiongozwa na katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji ndugu Mwinjuma Mkungu imefanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo iliyoetekelezwa kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 katika halmashauri kilwa katika kata za miguruwe na Njinjo ambapo miradi 6 yenye thamani ya Bilioni 1,16 imetembelewa na kukaguliwa . Miradi hiyo ni Ujenzi wa kituo cha Afya zinga gharama ni Milioni 600, Ujenzi wa zahanati ya njinjo na nyumba ya watumishi wa afya Milioni 249, Ujenzi wa mnada wa mifugo Milioni 100, ukarabati wa shule ya msingi kipindimbi 100, Ujenzi wa madarasa mawili 40, Ujenzi wa stand nangurukuru awamu ya pili, kutembelea mradi wa maji mavuji wenye thaman Bilioni 44, Ujenzi wa nyumba ya watumishi walimu 95, Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenz 220, Ujenzi wa mabweni mawili na madarasa manne 325. Aidha, timu hiyo ilipongeza juhudi za Halmashauri hiyo katika kusimamia na kutekeleza miradi na kuwataka kuendelea kikamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.