Katika ufunguzi wa semina ya mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura, Makamu Mwenyekiti wa INEC Jaji wa Rufaa (Mst) Mbarouk S. Mbarouk amewaeleza Watendaji wa Uchaguzi Ngazi ya Mkoa kuwa Mawakala wa Vyama vya Siasa wanaruhusiwa kuwepo katika Vituo vya Uandikishaji licha ya kwamba hawaruhusiwi kuingilia majukumu ya watendaji wakati wote wa utekelezaji.
"Wakati wa Uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapigakura. Jambo hili ni muhimu kwani litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima na kusaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea vurugu zisizokuwa za lazima. Aidha, mawakala hao hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao vituoni" ameeleza.
Aidha, Jaji Mbarouk ameongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa Elimu ya Mpigakura inawafikia wananchi wote, Tume imetoa kibali cha kutoa Elimu ya Mpigakura wakati wa uboreshaji wa Daftari kwa asasi za kiraia 157 na asasi za kiraia 33 kwa ajiri ya uangalizi wa zoezi hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.