Akiwashukuru na kuwapongeza wadau wa Michezo Sport Development Finland na Sport Development Tanzania kwa kuendelea kutoa mchango wao katika kukuza michezo Mkaoni humo. Michango hiyo inasaidia sana maandalizi ya UMITASHUMTA na UMISETA.
Bi. Zuwena Omary Katibu Tawala Mkoa wa Lindi ametoa pongezi na shukrani kwa wadau hao wakati akaikabidhiwa vifaa hivyo Mei 20, 2025 ofisini kwake huku akiwasihii kuendeleaza jitahada hizo za kukuza michezo .
"Tunawashukuru Sports Development Finland na Sports Development Tanzania kwa namna ambavyo mmetushika mkono kwa swala zima la maendeleo ya maichezo , tumeendelea kupokea zawadi tumeendelea kupokea mafunzo na supoti wakati wote . Sisi ahadi yetu ni kwamba kupitia idara ya elimu tutaendelea kusimamia na kuhakikisha kwamba vifaa hivi vinatumika vizuri, lakini pia tunahakikisha tunaendeleza michezo mashuleni kwenye shule zetu na vijana kwa ujumla " Bi. Zuwena Omary
Vifaa hivyo vimetolewa katika kuunga jitihada za serikali za kuinua michezo.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi Ndugu Ramson Lukas ameeleza kuwa wamekuwa wakifanya kazi na wizara ya elimu ya kutoa vifaa vya michezo na mafunzo ambayo yanamjenga mwanafunzi kuwa bora zaidi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.