Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Lindi 2025 yamefungwa rasmi leo, tarehe 14 Juni 2025, wilayani Ruangwa, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, ameishukru Serikali, wadau na wananchi wote walioshiriki na kuwezesha mafanikio makubwa ya tukio hilo.
Katika salamu zake, Mhe. Telack ameeleza kuwa maonesho hayo yamekuwa daraja muhimu la kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo na kutoa elimu ya kitaalamu kwa wadau wa sekta ya madini, huku akisisitiza dhamira ya Serikali ya Mkoa kuendelea kusimamia na kutangaza fursa zilizopo ili kukuza uchumi wa wananchi.
“Lindi ni Mkoa wa kukimbilia, si wa kutembea, tunahitaji kasi na mshikamano ili kila mmoja afaidi rasilimali tulizonazo, tutaendelea kutangaza fursa hizi kwa nguvu zote,” amesema Mhe. Telack.
Aidha, Maonesho hayo ya siku nne yaliyoanza tarehe 11 Juni 2025, yalifunguliwa na Mhe. Shaib Hassan Kaduara Waziri wa Maji Nishati na Madini kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.
Kwa mujibu wa Mhe. Telack, zaidi ya washiriki 86 kutoka sekta ya umma na binafsi wameshiriki, huku maonesho hayo yakivuta zaidi ya wananchi 7,000 waliokuja kuona teknolojia, bidhaa na huduma mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa sekta ya madini.
Katika kipindi cha maonesho, kulifanyika pia mafunzo ya kitaalamu yaliyolenga kuboresha uelewa na uwezo wa wachimbaji, huku yakiwa kichocheo cha mabadiliko chanya na washiriki wamepata ujuzi wa kipekee utakaowasaidia kuboresha shughuli zao kwa tija na usalama.
Mbali na hayo, Mhe. Telack ametumia jukwaa hilo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya madini na huduma za kijamii mkoani Lindi.
“Ninamshukuru sana Mhe. Rais kwa kutuamini na kuwekeza fedha nyingi katika Mkoa wetu, ikiwemo madaraja yaliyoharibiwa na mvua ambayo sasa wakandarasi wamelipwa na wanaendelea na kazi,” amesema Mhe. Telack.
Sambamba na hayo, ametoa pongezi kwa wadhamini wakuu wa maonesho akiwemo ELIANJE GENESIS CO. LTD, UVIWAMA, LINDI JUMBO, MINERAL ACCESS, PMBET na SI
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.