Chama kikuu cha ushirika Lindi Mwambao kimekabidhi madawati 150, Matairi ya Gari Manne na Viti mwendo viwili kwa ajilia ya kutimiza nguzo ya saba kwa kurejesha faida kwa jamii.
Akipokea vifaa hivyo kwaniaba ya wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva amekipongeza chama kikuu cha ushirika Lindi Mwambao kwa kurejesha faida kwa jamii .
“Naombeni mpokee salamu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack anatambua na kuthamini kazi kubwa mnayofanya , kazi yenu ni nzuri, kazi yenu ni njema lakini mmekuwa chombo cha kuunganisha vyama vyetu vya msingi, na wakulima wetu , mmekuwa chombo cha kuhakikisha wakulima wanapata haki zao, nawapongeza bodi, Makamu mwenyekiti, meneja na stafu wote kwa kufanya kazi kubwa sana” - Amesema Dc Mwanziva.
Madawati hayo yatakwenda kutumika katika shule za msingi, Matairi kwa ajili ya gari la jeshi la Polisi na Viti mwendo kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Ofisi ya Lindi Mwambao iliyopo Mitwero kata ya Rasbura Manispaa ya Lindi leo Novemba 20, 2024 ,
Mhe.Mwanziva ametumia fursa hiyo kuwasihii wananchi kuhakikisha wana shiriki kusikiliza sera za wagombea ambao wanawania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024. Kampeni hizo zimeanza leo tarehe 20 mpaka 26 Novemba 2024.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Lindi Mhe. Frank Magali amempongeza Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri katika sekta ya Kilimo ambayo imeboresha maisha ya wakulima kuwa mazuri.
@owm_tz
@wizara_ya_kilimo
@lindi_mwambao_official
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.