Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary amewataka wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale kushirikiana na watumishi wenzao waliopo kwenye idara na vitengo hivyo kuweka mikakati madhubuti ili kukamilisha miradi kwa wakati.
‘’Wakuu wa idara wote wana wasaidizi wao ukishapata mradi kwenye idara yako pamoja na sekta zingine ambazo utakuwa unashirikiana nazo kama mipango, wewe unatakiwa uwe na mikakati ya ndani na wana idara wenzako ili miradi ikamilike kwa wakati’’ Katibu Tawala MKoa.
Aidha Bi. Zuwena amewataka wakuu wa idara hao wanapokuwa na mradi kuwa na utaratibu wa kufanya vikao na Menejimenti kwa kila wiki au mwezi na kutoa mrejesho kwa Mkurugenzi ili miradi imalizike kwa wakati.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe. Goodluck Mlinga ameliasa Baraza la madiwani kutoa ushirikiano katika kutokomeza utoro mashuleni.
Dc Mlinga ameongeza kuwa katika kuhakikisha utoro mashuleni unakomeshwa aliwaagiza viongozi wa Serikali za vijiji vyote kutengeneza sheria ndogo kwa ajili ya kuwadhibiti watoto na wazazi ambao hawataki kupeleka watoto shuleni.
Hayo yamesemwa leo Juni 16. 2025 katika Baraza maalumu la kujadili hoja za mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa hesabu za mwaka 2023-2024.
@ortamisemi
@liwaledc
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.