MAAFISA MAENDELEO YA JAMII LINDI WAPIGWA MSASA
Bwana. Alestida Kakulu, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamil, Jinsia na Makundi Maalum amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoani Lindi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi ili kutimiza adhima ya kuwa kitovu cha maendeleo katika jamii.
Kakulu ameyaeleza hayo wakati wa Kikao kazi cha Waataalamu wa Maendeleo ya Jamii Ngazi ya Mkoa kinachofanyika leo Disemba 04, 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Dockyard uliopo katika Manispaa ya Lindi.
Ameeleza kwamba, Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa sekta zinazobeba matarajio mengi ya katika jamii na yenye majukumu mengi zaidi ya kushughulika na vikundi vya mikopo ya 10%, hivyo, ni wajibu wa kila Afisa Maendeleo kutambua, kutekeleza majukumu na kuonyesha ustawi.
Vilevile, Kakulu amesisitiza kuwa Maafisa maendeleo ya Jamii wanatarajiwa kuwa mstari wa mbele kubadili fikra na mitazamo ya Jamii ikuwa chanya na kuendana na kasi ya mabadiliko na kuwa kitovu cha maendeleo.





Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.