Katika kufikia lengo la Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuhakikisha uzalishaji wa mazao ya kimkakati unaongezeka ikiwemo zao la Korosho, Bodi ya korosho Tanzania (CBT) imetoa mafunzo ya kuwajengea uelewa vijana kupitia program ya jenga kesho iliyobora (BBT) ili kuweza kufikia malengo ya Serikali kuzalisha Tani Milion 1 ifikapo 2030 .
Hayo yameelezwa na Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoa wa Lindi Ndugu Ramadhani Khatibu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ambayo yatafanyika kwa muda wa siku Tano.
"Mafunzo wanayoyatoa Bodi ya korosho ni kuwajengea uwezo maafisa kilimo katika kusimamia pembejeo,viwatilifu pamoja na kwenda kufufua mashamba pori ilikuweza kuongeza tija ya uzalishaji wa zao la korosho."Amesema Khatibu
Kwa pande wake mwakilishi kutoka bodi ya korosho George Nyaga amesema kuwa lengo la Serikali ifikapo 2030 uzalishaji uongezeke kufikia Tani Milioni moja, ambapo kwasasa korosho inayozalishwa nchini imefikia Tani laki 4.
Nyaga amesema kuwa kupitia programu ya BBT bodi ya korosho imeweza kuajiri vijana ambao ni wataalamu wa kilimo 500 na kuwapa mafunzo ambayo yatawasaidia wakulima walime kisasa na kuongeza uzalishaji wa zao la korosho, moja ya jukumu kubwa ambalo wanakwenda kuanza nalo ni kuisaidia bodi ya korosho kupata kanzu data ya wakulima na kwenda kufufua mashamba pori.
"Bodi ya korosho kupitia program ya BBT tumeweza kuajiri vijana 500 na kuwapeleka katika mikoa ambayo inazalisha korosho kwa wingi,ikiwemo Lindi,Mtwara,Pwani,Ruvuma na Tanga."Amesema Nyaga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.