Maelfu ya watu wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika kilele cha Maonesho ya Madini Mkoa wa Lindi yanayofanyika katika Viwanja vya maonesho ya madini vilivyopo Kilimahewa, wilayani Ruangwa leo tarehe 14 Juni, 2025.
Mahudhurio hayo makubwa yanajumuisha viongozi wa Serikali, viongozi wa dini, vyama vya siasa na wananchi wa Mkoa wa Lindi, pamoja na wageni kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwa ni ishara ya mwitikio chanya na hamasa kubwa kutoka kwa jamii kuhusu nafasi ya sekta ya madini katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Aidha, kilele cha maonesho hayo kimeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wa kada mbalimbali, wajasiriamali, wanafunzi na wadau wa maendeleo, huku shughuli mbalimbali zikiendelea viwanjani tangu asubuhi.
Ikumbukwe, maonesho haya ni sehemu ya mkakati wa Mkoa wa Lindi kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika uchumi wa madini na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.