MAMIA WAMIMINIKA BANDA LA OFISI YA MKUU WA MKOA WA LINDI -MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM (SABASABA) .
Julai 7, 2025 Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ( Sabasaba ) yamefunguliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussen Ali Mwinyi huku mamia wakitembelea banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kushuhudia utajiri, fursa, bidhaa na mali zilizopo Mkoani humo na kupata elimu mbalimbali.
Wajasiriamali kutoka Halmashauri za Mkoa wa Lindi wameshiriki maonesho hayo wakiwa na bidhaa mbalimbali zikiwemo zile zinazotokana na bahari kama vile mwani .
Maonesho hayo yanayofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Wote mnakaribishwa sana .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.