Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amewakaribisha wananchi na wadau wa madini wote wa ndani na nje ya nchi katika maonesho ya Madini na fursa za uwekezaji . ( 2nd Lindi Mining Expo 2025 ).
"Mkoa wa Lindi tunatarajia kufanya Maonesho ya pili ya Madini tarehe 11 mpaka tarehe 14 mwezi wa sita, Maonesho haya yatafanyika kwenye viwanja vya madini vilivyopo wilaya ya Ruangwa na yataandamana na ratiba mbalimbali" Mhe. Telack rC Lindi.
Mhe. Telack amesema kuwa Maonesho hayo ya pili ya Madini yanatarajiwa kuambatana na shughuli mbalimbali ambazo zitakuwa na tija zaidi kwa yeyote ambaye anavutiwa, anajishughulisha ama anatarajia kujishughulisha na madini hivyo kila mwananchi na mdau wa madini aone fursa ya kushiriki Maonesho hayo muhimu kwa Mkoa na Taifa kwa ujumla .
"Nitumie nafasi hii kuwakaribisha wote ambao wanafanya shughuli za madini wanaochenjua, wanaonunua, wanaochimba waje kwenye maonesho hayo ili kuona fursa mbalimbali zilizopo za Madini zilizopo Mkoa wa Lindi.
Ameongeza kuwa katika Maonesho hayo kutakuwa na wafanya biashara wa iana zote wakubwa na wadogo hivyo ni sehemu muhimu sana ya kukutana na wadau mbalinbali.
Aidha, Mhe. Telack ametaja baadhi ya Madini ambayo yanapatikana zaidi Mkoa wa Lindi pamoja na Dhahabu, kinywe (Graphite), Mabo ya blue ambayo tanzania yanapatikana sehemu chache sana na Nikel .
Amesisitiza kuwa makampuni yenye mitambo na vifaa mbalimbali ya uchimbaji wa madini wanakaribishwa zaidi kwani wachimbaji wengi hasa wadogo hawafahamu baadhi ya vifaa na namna ya kuvipata na kuvitumia.
Ameeleza kuwa Maonesho haya ni namna ya kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha mazingira rafiki ya uwekezaji, kuinua uchumi wa wananchi na taifa kupitia sekta ya madini.
Kauli Mbiu ya Maonesho haya inasema " Madini na Uwekezaji Fursa ya Kiuchumi Lindi, Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 ?
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.