Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amesema kuwa mkoa wa Lindi umebarikiwa kuwa na ardhi yenye utajiri mkubwa wa madini mbalimbali, jambo ambalo limeanza kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa wakazi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika uzinduzi wa Maonyesho ya Madini Msimu wa Pili yaliyofanyika katika viwanja vya madini wilayani Ruangwa, RC Telack alieleza kuwa maonesho hayo yanafungua fursa nyingi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, huku yakichochea shughuli za uchumi na kuongeza thamani ya madini yanayochimbwa katika maeneo mbalimbali ya Lindi.
“Kwa sasa tunaona wawekezaji wakikimbilia kuwekeza katika sekta ya madini hapa Lindi, jambo ambalo linachochea maendeleo ya kiuchumi, uboreshaji wa miundombinu, pamoja na fursa za ajira kwa wananchi wetu,” alisema RC Telack.
Aidha, Telack alibainisha kuwa maonesho ya awamu ya kwanza yalipata mafanikio makubwa baada ya kuhudhuriwa na wageni kutoka nchi 14, jambo ambalo limeyafanya kuwa maonyesho ya kimataifa na kuongeza mvuto wa mkoa wa Lindi kama kitovu kipya cha shughuli za madini nchini.
“Lindi sasa inajitokeza kama mkoa wa kimkakati katika sekta ya madini, na tuna kila sababu ya kushirikiana kwa karibu na wawekezaji ili kuhakikisha tunaendeleza rasilimali hizi kwa manufaa ya Watanzania wote,” aliongeza.
Maonyesho hayo yanatarajiwa kudumu kwa siku Nnr huku yakihusisha maonesho ya bidhaa za madini, teknolojia za uchimbaji, warsha za kitaalam pamoja na majadiliano baina ya serikali, wawekezaji na wachimbaji wadogo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.