Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo Bwana. Wilson Nene amesema kuwa zaidi ya asilimia 76 ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo, hivyo sekta hii ina nafasi kubwa katika kukuza uchumi na ustawi wa jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, amesema serikali imeweka mikakati madhubuti ya kutekeleza Ajenda 10/30, inayolenga kuhakikisha sekta ya kilimo inachangia kikamilifu kwenye pato la taifa.
“Mojawapo ya mikakati hiyo ni kupitia maonesho ya Nanenane kama haya, ambapo teknolojia mbalimbali huoneshwa kwa wakulima na wadau ili waweze kuzipokea na kuzitumia kuongeza tija kwenye uzalishaji wa mazao,” alieleza.
Ameongeza kuwa Wizara ya Kilimo imejipanga vyema kushiriki kikamilifu maonesho haya, na inawatakia kila la heri wananchi wote wanaoyatembelea. Ameeleza matumaini kuwa teknolojia zitakazopatikana zitaleta mabadiliko chanya katika kilimo, na kusaidia kufanikisha ajenda ya mageuzi ya kiuchumi kupitia kilimo bora.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.