Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Shaibu Hassan Kaduara, amezindua rasmi awamu ya pili ya Maoneesho ya Madini (Lindi Mining Expo) mkoani Lindi, yakilenga kuvutia wawekezaji na kutangaza fursa mbalimbali za rasilimali madini zinazopatikana mkoani humo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Kaduara alisema thamani ya dhahabu imeendelea kupanda katika soko la dunia kutokana na athari za vita kati ya Urusi na Ukraine, ambako dhahabu inayozalishwa na Urusi imewekewa vikwazo kuingia katika masoko ya kimataifa.
"Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya 1996, pamoja na Sera ya Maendeleo ya Viwanda ya 1996–2020 na ile ya Viwanda Vidogo ya mwaka 2003, zipo kwenye mchakato wa kupitia upya kwa lengo la kuendana na mahitaji ya sasa ya maendeleo ya kimkakati," alisema Kaduara.
Waziri huyo alibainisha kuwa miradi ya madini ni miongoni mwa miradi ya kimkakati nchini, ambayo inaendelea kufanyiwa tathmini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sera mpya itakayowezesha Watanzania kunufaika zaidi na sekta hiyo.
Lindi yajitokeza Kama Kitovu cha Madini Nchini
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Zainab Telack, alisema mkoa huo umebarikiwa kuwa na rasilimali kubwa za madini ambazo tayari zimeanza kuwanufaisha wananchi moja kwa moja.
“Maonesho haya yanafungua milango kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Yanachochea uchumi wa eneo hili na kuongeza thamani ya madini tunayochimba,” alisema RC Telack.
Aliongeza kuwa maonesho ya awamu ya kwanza mwaka 2023 yalivutia wageni kutoka mataifa 14 na zaidi ya watu 6,000 walihudhuria, jambo lililoongeza hadhi ya Lindi kama eneo la kimkakati kwa shughuli za madini nchini.
“Kwa sasa tunaona ongezeko la wawekezaji, uboreshaji wa miundombinu na fursa za ajira, hali inayodhihirisha kuwa Lindi ni sehemu muhimu katika ajenda ya maendeleo ya taifa,” aliongeza.
Ongezeko la Wachimbaji na Teknolojia ya Uchimbaji
Kwa mujibu wa Mratibu wa Maonyesho hayo, Bw. Mwinjuma Mkungu, ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi mkoani Lindi, idadi ya wachimbaji imeongeka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.