Kufuatia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Lindi kutangaza kusitisha matumizi ya Barabara inayounganisha mikoa ya kusini kutokana na kukatika kwa daraja la dharura Somanga Mtama leo April 6, 2025.
Meneja wa TANAROADS Mkoa wa Lindi, Mhandisi Emil Silas Zengo amesema kuwa zoezi la kurejesha mawasiliano ya barabara yanafanyika usiku na mchana lengo kuhakikisha hadi kufikia April 7, Jioni (kesho) mawasiliano ya barabara yanarejea .
"Maji sasa hivi yamepungua kiasi fulani, lakini bado mengi, ila sasa hivi tunataka tuanze kupafanyia kazi, serikali hailali, mpaka kesho jioni tumejiwekea tuwe tumeshafungua " Alisema Mhandisi Zengo .
Mhandisi Zengo ameyasema hayo leo April 6, 2025 majira ya saa 03:30 Usiku akizingumza kwa njia ya Simu na Afisa Habari Mkoa .
Aidha, Wito kwa wananchi na watumiaji watumiaji wa vyombo vya moto kuendelea kuwa watulivu wakati zoezi la kurejesha mawasiliano ya eneo husika likiendelea .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.