MFUMO WA BEI NA MINADA NI USHINDANI HALISI UNAOTOKANA NA SOKO HURU LA KIMTANDAO- DC NGOMA
Chama Kikuu cha Ushirika cha RUNALI kimeendesha mnada wake wa kwanza wa zao la korosho kwa msimu wa 2025 kwa mafanikio baada ya wakulima kutoka katika Wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale kuridhia kuuza Kg. 20, 630, 516 za korosho kwa bei ya juu ya Sh. 2,610 na ya chini Sh. 2,460 kwa kilo.
Akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma amesisitiza kuwa bei na mfumo wa mnada unatokana na soko huru la mtandaoni unaoleta ushindani wa kweli na kuzitaka mamlaka zinazohusika kushughulikia mapema malipo ya wakulima ili waweze kupata fedha zao kwa wakati.
"Tunasisitiza na kukumbushana kuwa bei na mfumo na kuuza inatokana na soko huru la mtandaoni unaotokana na ushindani halisi, tunavyopata bei nzuri ni bei halisi ya soko. Tunaenda kupokea fedha kwa pamoja, tusaidizane kwenye uadilifu, tukatumie kwa matumizi yetu na kwa ajiri ya maandalizi ya msimu ujao" Mhe. Ngoma.
Bi. Consolata Kiruma, kwa niaba ya Mrajisi Mkuu wa Vyama vya Ushirika amewashukuru wakulima waliohudhuria na kufanikisha mauzo hayo na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kusimamia ubora wa korosho, hususan katika hatua ya ukaushaji ili kufikia viwango vya soko la kimataifa.
"Tuzingatie ubora kama tunavyoelekeza na wataalamu ili tuendelee kutunza sifa za mazao yanayopokelewa na vyama vyetu, Wilaya na Mkoa. Katika vyama vyetu tuzingatie misingi, maadili, uaminifu na uadilifu ili viendelee kuaminika na kuimarika. Kila mmoja kwa nafasi yake atimize wajibu wake" amesisitiza Bi. Amina Njoro, mkulima kutoka Ruangwa amesema,
“Mnada wa leo umetupatia matumaini, tunaiomba serikali iendelee kuimarisha utendaji wa vyama vyetu ili wakulima wanufaike zaidi. Bei imekua nzuri na tumeikubali tunaomba serikali izidi kutusimamia kupitia mfumo huu” Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho (CBT), Francis Alfred, amewapongeza wakulima wote walioshiriki mnada huo na kuwataka kuendelea kusimamia ubora na thamani ya zao la korosho kwa ustawi endelevu wenye tija hususan katika hatua ya ukaushaji wa korosho ili kuweza kupata korosho yenye tija na ubora unaokidhi viwango na mahitaji ya soko.








Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.