Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew amefanya ziara ha kikazi katika Mkoa wa Lindi ambapo ameanza kwa kukutana na watumishi wa sekta za mamlaka ya maji mkoa wa Lindi na kuziagiza mamalaka Mamlaka za maji nchini kuacha tabia ya kuwakatia maji wateja wao pamoja na kuwatoza faini wateja wanaohitaji kurejeshewa huduma ya maji badala yake waone namna ya kuunganisha wateja mita za kisasa ambazo wanalipia huduma ya maji kadri wanavyotumia.
Akizungumza na watumishi hao kwenye kikao cha sekta ya maji kilichounganisha Mamlaka za maji mkoani Lindi,Bonde la mto Ruvuma, Pwani ya kusini na Maabara ya ubora wa maji kanda ya Mtwara, Mhandisi Mathew amezipongeza mamlaka hizo kwa kazi nzuri na kubwa wanayoifanya ya kusimamia miradi mikubwa na ya kimkakati ya maji pamoja na kuunganisha mtandao wa maji safi na salama katika maeneo ya mijini na vijijini na kupelekea upatikanaji wa maji katika maeneo ya mijini kwa asilimia 61 na vijijini asilimia 63 katika mkoa wa Lindi.
Aidha, Mhandisi Kundo amesisitiza kuhusu kupanga mipango madhubuti inayoweza kutekelezeka, usimamizi na uendelezaji wa utoaji wa huduma ili iweze kuondoa manung'uniko na malalamiko ya wananchi katika utoaji wa huduma za sekta ya maji pamoja na kufanya utafiti wa kuziba mapungufu yanayoweza kujitokeza katika utoaji wa huduma kulingana na kuongezeka kwa watumiaji wa maji.
Aidha, Meneja wa Wakala wa maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa)Mkoa wa Lindi, Mhandisi Muhibu Lubasa amesema kuwa Mkoa unaendelea na utekelezaji wa miradi ya Maji mikubwa na Midogo 7 yenye gharama ya jumla ya Tsh. Bilioni 64.5 ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji pamoja na miradi mingine 16 ikiwemo mradi wa vijiji 16, pamoja na utekelezani wa visima vya majimbo jumla 35 pamoja na vioksi 35 katika kila jimbo la uchaguzi ambapo visima 32 tayari vimeshajengwa na vimekidhi vigezo vyote vinavhohitajika ili vianze kuhudumia kwa kutoa maji kwa wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.