Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, ametembelea na kukagua Miradi mbalimbali inayotarajiwa kupitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu wilayani Ruangwa, ambapo ameonesha kuridhishwa na maendeleo yake.
Miradi hiyo inajumuisha ujenzi wa Barabara ya Mwilahi yenye urefu wa mita 650 katika Kijiji cha Likangara wenye thamani ya zaidi ya Tzs Milioni 513, Mradi wa Dampo Salama wa kikundi cha vijana wa usafi wa mazingira katika Kijiji cha Lipande wenye thamani ya Tzs Milioni 15, na Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na Ofisi moja katika Shule ya Msingi Dodoma, Kata ya Nachingwea wenye thamani ya Tzs Milioni 48.
Aidha, Miradi mingine inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru ni pamoja na:
Mradi wa Maji wa Kijiji cha Mpara, Kata ya Likunja, unaohusisha uchimbaji wa visima na ujenzi wa miundombinu ya maji kwa thamani ya zaidi ya TZS 325 milioni.
Ujenzi wa Kituo cha Polisi Nandagala, wenye thamani ya TZS 164 milioni.
Ujenzi wa Kituo cha Afya Namakuku, ambapo Mwenge wa Uhuru utaweka jiwe la msingi kwenye jengo la OPD lenye thamani ya zaidi ya TZS 153 milioni.
Ujenzi wa Shule ya Sekondari Namakuku, ambapo Mwenge utaweka jiwe la msingi kwenye mradi wenye thamani ya zaidi ya TZS 591 milioni.
Kwa mujibu wa ratiba, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa Mei 28 katika Kijiji cha Namichiga, ambapo utapitia miradi hiyo na hatimaye kulala katika Kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa.
@ortamisemi
@owm_tz
@ofisi_ya_makamu_wa_rais
@maelezonews
@nchikwanza
@samia.app
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.