Mkoa wa Lindi umepokea mwenge wa Uhuru kutoka mkoa wa Mtwara ambapo kwa mkoa wa Lindi utakimbizwa km 999.7,kwa Halmashauri sita zilizopo mkoani huo.
Akizungumza leo Jumatatu Mei 26,2025 mara baada ya kuupokea Mwenge wa Uhuru, mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amesema kuwa miradi itakayo tembelewa na mwenge wa uhuru kwa mkoa wa Lindi ni miradi 59,yenye thamani ya Sh.22.4 Bilioni.
Telack ameendelea kusema kuwa miradi hiyo 19 itawekwa mawe ya msingi ,6 itazinduliwa na 34 itatembelewa na kuonwa.
"Mwenge wa uhuru utakimbizwa mkoani kwetu katika Halmshauri sita za mkoa wa Lindi ,na miradi yote itakayopitiwa na mwenge wa uhuru ni miradh 59 yenye thamani ya Sh.22.4Bilioni."amesema Telack
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva wakati akikabidhiwa mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telack amesema kuwa mwenge wa uhuru kwa Halmashauri ya Mtama utakimbizwa km 105 na itakagua ,kuona na kuzindua miradi 7 yenye thamani ya Sh.2bilioni.
"Tutakimbiza mwenge wa uhuru kwenye Halmashauri yetu ya Mtama umbali wa km 105na utazindua ,kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi 7 yenye thamani ya Sh.bilioni 2"amesema Mwanziva.
Mwanziva amewataka wananchi wa Halmashauri ya Mtama kujitokeza kwa wingi katika maeneo yao pindi mwenge wa uhuru ukiwa unapita.
"Niwaombe wananchi wa Halmashauri ya Mtama kujitokeza kwa wingi kwenye maeneo yetu ili kuulaki pindi mwenge wa uhuru ukiwa unapita ."amesema DC Mwanziva
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.